Nalipaje?
Baada ya kujisajili utaona Lipa Namba na kiasi. Lipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au benki, kisha weka namba ya muamala kwenye ukurasa wa usajili wako.
Nitapata lini namba ya uanachama?
Tukishathibitisha malipo — kwa kawaida siku hiyo hiyo ya kazi — utapokea SMS yenye namba yako ya uanachama.
Nijiandae vipi kwa vipimo?
Usile chochote masaa 8–12 kabla (maji ni sawa). Njoo na kitambulisho na kadi yako ya BMI Afya Kwanza.
Majibu yangu yatakuwa tayari lini?
Kwa kawaida ndani ya siku 3 za kazi baada ya vipimo. Mtaalamu huyapitia na kukuandikia mpango wa afya, kisha utapokea SMS.
Siwezi kuingia.
Tumia namba ya simu uliyotumia kujisajili. Code inatumwa tu kama malipo yako yamethibitishwa. Bado shida? Tupigie.
BodyMind Insights Consultation Clinic · Usajili Wizara ya Afya Na. 125773-2